Saturday, February 2, 2013

RONALDO AUMIA ENKA, SHAKANI KUWAVAA MAN U

Ronaldo akishikilia enka yake iliyoumia

JERAHA la enka alilonalo Cristiano Ronaldo linamaanisha kwamba atacheza mechi yao ya leo ya La Liga dhidi ya Granada akiwa amevaa kifaa maalum cha kusapoti enka na hiyo ni kama atachezeshwa.

Mreno huyo alisafiri kwenda Granada akiwa na onyo kwamba atajihatarishia jeraha kubwa zaidi na anaweza akajikuta akikosa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya timu yake ya zamani ya Manchester United. Zimebaki siku 11 tu.

Kocha Jose Mourinho ndiye mwenye maamuzi ya mwisho. Anaweza kumteua katika kikosi cha kwanza na kisha asimchezeshe mechi yote, au akamuanzisha benchi na kumtumia baadauye kama mambo yatakuwa hayaendi. Kwa kuwa mechi itachezwa usiku, Ronaldo anaweza kuitumia siku nzima ya leo kufanya kazi na daktari wa viungo kwa ajili ya kumsaidia kupunguza maumivu. Lakini kinachofahamika ni kwamba kama atacheza, atavaa kifaa maalum cha kukinga  enka.

Ronaldo alipata majeraha hayo katika kipindi cha pili cha mechi yao ya Jumapili dhidi ya Getafe, wakati alipokimbia kwa mwendo mrefu kuelekea golini, na akasimamishwa na Borja Varela. Alicheza akiwa na majeraha hayo wakati alipowakabili Barcelona ambapo alivaa kifaa hicho ambacho antarajiwa kukitumia leo. Ni aina ya plasta ambayo inasapoti kiungo, lakini inaweza kumzuia kucheza kwa kasi yake ya kawaida
.

No comments:

Post a Comment