Saturday, February 2, 2013

PEPE APONA, HUENDA AKAWAVAA MAN UTD... AANZA KUJIFUA NA MPIRA

Pepe

BEKI wa Real Madrid, Pepe anatarajiwa kurejea uwanjani mapema kuliko ilivyotarajiwa baada ya kushiriki mazoezi mazito jana Ijumaa.

Mazoezi ya jana yalichukua nusu saa tu lakini yalijumuisha mazoezi ya viungo na kuchezea mpira ambayo aliyafanya peke yake. Hatimaye mwanga wa matumaini umeanza kuonekana kwa beki huyo Mreno.

Enka yake ilionekana kuwa poa wakati akikimbia na kupiga mpira na huenda wiki ijayo akaanza kujifua pamoja na wachezaji wenzake baada ya kuachwa nje ya kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kitakachocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ecuador Jumatano mjini Guimaraes.

Ni mwezi sasa tangu alipofanyiwa upasuaji wa enka mjini Porto. Baada ya miezi kadhaa ya kucheza na maumivu kuelekea Desemba, beki huyo mwenye mwili "kabati" huenda akarejea kikosini katika mechi ya wiki ijayo dhidi ya Sevilla. Hiyo itakuwa ni kabla ya mechi yao dhidi ya Manchester United, ambayo anatarajiwa kuchuana na Rooney, VanPersie na wenzao.

Hata hivyo, kiwango cha juu alicho nacho beki yosso Raphael Varane, hasa alichoonyesha katika mechi ya Jumatano dhidi ya Barcelona, kitampunguzia presha kocha Jose Mourinho kwa kiwango fulani, na anaweza asihitaji kumuwahisha Pepe kurejea kabla ya muda aliofikiria.

No comments:

Post a Comment