Sunday, February 17, 2013

REAL MADRID YAANZA MCHAKATO KUTAKA KUMSAJILI 'KIBERENGE' GARETH BALE WA TOTTENHAM ... YADAIWA RAIS FLORENTINO PEREZ YUKO TAYARI KULIPA BIL. 123/-

Gareth Bale
LONDON, England
Real Madrid wameanza rasmi kumfukuzia winga nyota wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya England, Gareth Bale.

Gazeti la Sunday Telegraph limesema leo kuwa Real Madrid wameitaka Tottenham iwaambie kama wako tayari kuwauzia Bale, wakati rais wa mabingwa hao wa Hispania, Florentino Perez akidaiwa kuwa tayari kumwaga paundi za England milioni 50 (bilioni 123.4) ili kumnasa mchezaji huyo anayetajwa kuwa ndiye bora zaidi kuliko wote kwa sasa katika Ligi Kuu ya England.

Real Madrid walielezea nia yao ya kumtwaa Bale wakati wakimsajili Luka Modric kutoka Tottenham katika kipindi kilichopita cha uhamisho wa majira kiangazi na sasa wameomba kupewa nafasi ya kumsajili mara tu watakapokuwa tayari kumuuza.

No comments:

Post a Comment