Lionel Messi akifunga goli la kwanza kwa mguu wa kulia dhidi ya Granada usiku wa kuamkia leo |
Messi akifunga goli la kwanza dhidi ya Granada |
Messi akishuhudia mpira aliopiga ukitinga wavuni |
Kitu ndani ya wavu |
Cesc Fabregas akichana katikati ya wachezaji wa Granada |
Napita humu humu... Lionel Messi akipita katikati ya mabeki wa Granada |
Hatariiii... Lionel Messi akifunga goli la pili kwa 'fri-kiki' moja matata sana |
Lionel Messi akishangilia goli lake la pili |
Messi akishangilia goli lake la pili |
Messi akishangilia goli lake la pili pamoja na wachezaji wenzake wa Barca |
Messi (10) akishangilia goli lake la pili pamoja na wachezaji wenzake wa Barca |
Messi akiukosa mpira wakati akijaribu kufunga langoni mwa Granada |
NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi alifunga magoli mawili na kuipa timu yake pointi tatu dhidi ya Granada usiku wa kuamkia leo.
Messi alifunga goli lake la 300 na la 301 tangu aanze kuichezea Barcelona wakati vinara hao wa La Liga walipozinduka kutoka 1-0 nyuma wakati wa mapumziko na kushinda 2-1 ugenini dhidi ya Granada.
Barca walitawala kwa dakika 25 za kwanza, lakini walishangazwa wakati Odion Ighalo alipowafungia wenyeji goli la kuongoza kwenye Uwanja wa Nuevo Los Carmenes.
Messi alidokolea wavuni goli walilostahili la kusawazisha katika dakika ya 50 na kisha akafunga kwa 'fri-kiki' ya hatari sana iliyokwenda moja kwa moja wavuni dakika 17 kabla ya mechi kumalizika na kuifanya Barca iongoze kwa tofauti ya pointi 15 juu ya Atletico Madrid na pia pointi 19 juu ya Real Madrid kabla ya mechi zao za usiku wa leo.
Akiwa na umri wa miaka 25 tu, Messi tayari amefunga magoli 301 akiwa na klabu hiyo ambapo magoli 206 amefunga katika 'La Liga', 24 Kombe la Mfalme, 10 kwenye Spanish Super Cup, 56 kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, manne kwenye Kombe la Dunia la Klabu na moja kwenye European Super Cup.
Kilichovutia zaidi ni kwamba alifunga goli hilo kwenye uwanja wa Los Carmenes, ambao kufikia sasa ulikuwa haujaonja goli la Messi.
Kufuatia magoli hayo dhidi ya Granada, katika mechi yake ya 365 akiwa na Barcelona, inamaanisha kwamba amebakisha uwanja mmoja tu ambao hajafunga goli wa Cornella-El Prat wa mahasimu wao wa mji mmoja wa Espanyol. Kama Messi atafunga goli hapo atakuwa amefunga katika kila uwanja wa klabu zote zilizopo kwenye Ligi Kuu ya Hispania hivi sasa.
Na zaidi, Messi ameendeleza rekodi yake ya kufunga katika mechi 14 mfululizo na ni mchezaji wa kwanza katika historia ya 'La Liga' kufunga katika mechi 10 mfululizo za ugenini.
Messi hivi sasa anaongoza 'ligi' ya wafungaji wa 'La Liga' akiwa na magoli 37, yanayomweka katika nafasi nzuri ya kuivunja rekodi yake mwenyewe aliyoiweka mwaka jana ya kufunga magoli 50 katika Ligi Kuu, hasa ukizingatia kwamba kuna mechi 14 bado za kucheza hadi mwisho wa msimu.
No comments:
Post a Comment