Saturday, February 2, 2013

MESSI ALITEMEA MATE BENCHI LA REAL MADRID?

Alvaro Arbeloa akimpa "shughuli" Messi kabla ya wawili hao kudaiwa kubwatukiana kwenye maegesho ya magari ya Real Madrid, ambako Messi alidaiwa kumfuata Arbeloa na kwenda kumbwatukia wakati beki huyo akiwa kwenye gari yake na mkewe.

MECHI ya 'El Clásico' inaendelea kutawala vichwa vya habari huku Lionel Messi akiendelea kuwa mjadala.

Baada ya mjadala wa kubwatukiana na Alvaro Arbeloa, sasa imepatikana video inayomuonyesha Muargentina huyo mwenye mwili "mduchu" akitema mate kuelekea upande wa benchi la Real Madrid wakati wa mechi.

Video hizo zilizochukuliwa kutoka katika vituo vya televisheni vya Hispania vya 'La Sexta' na 'Cuatro', zinamuonyesha Messi akitema mate wakati wa mechi ikiendelea Jumatano usiku.

Hata hivyo, jambo ambalo haliko wazi ni uelekeo gani alitemea mate hayo mchezaji huyo wa Barca ambaye alikuwa mbele ya benchi la Real Madrid. Ni vigumu kubaini kama mchezaji huyo alijaribu kuwatemea mate watu waliokuwa katika benchi hilo au haikuwa dhamira hiyo.

Kinachoonekana katika video ya La Sexta ni namna Messi anavyojibizana na mtu aliyekuwa katika benchi la Madrid, pengine mmoja wa makocha ama mchezaji wa akiba, wakati video ya Cuatro inamuonyesha wazi akitema mate.

No comments:

Post a Comment