Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete |
Vigogo wanaotajwatajwa kuwa wana 'usongo' wa kuwania urais mwaka 2015 kama waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernad Membe, wameachwa ndani ya chombo hicho cha juu zaidi, ambacho huwa kina wajumbe saba kutoka Bara na wengine wa idadi hiyo kutoka Zanzibar.
Kwa kawaida, majina ya wajumbe hao hupendekezwa na mwenyekiti wa chama na hivyo, Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyewateua na wajumbe wa NEC kuwapitisha.
Majina ya wajumbe saba wa kamati kuu (CC) ya CCM waliopitishwa kutoka Bara ni:
1. Pindi Chana
2. Adam Kimbisa
3. William Lukuvi
4. Dk. Emmanuel Nchimbi
5. Jerry Slaa
6. Prof. Anna Tibaijuka
7. Stephen Wassira
Kutoka Zanzibar, wajumbe saba waliopitishwa katika CC ya CCM ni:
1. Shamsi Vuai Nahodha
2. Dk. Hussein Mwinyi
3. Prof. Makame Mbarawa Mnyaa
4. Dk. Salim Ahmed Salim
5. Dk. Maua Daftari
6. Samia Suluhu Hassan
7. Hadija H. Aboud
Kwa utaratibu wa CCM, wajumbe wa CC ndiyo wenye rungu la kuchuja majina ya wagombea wote wa urais kupitia chama hicho ambapo mwishowe hupeleka majina ya mwisho ya wale wote wenye sifa kwenye mkutano wa halmashauri kuu (NEC) ili hatimaye kubaki na mgombea mmoja anayepeperusha bendera ya chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu.
Hivyo, ni wajumbe hawa 14 ndiyo watakaoamua hatma ya wagombea urais wa CCM, kwani wanao uwezo wa kufyeka jina la mgombea yeyote kwa sababu watakazoona kuwa zinafaa wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu wa 2015 utakapoanza kwa kusaka wagombea ndani ya vyama, kikiwamo CCM.
No comments:
Post a Comment