Telephone: 255-22-2122771
E-mail: maelezopress@yahoo.com
|
Idara ya Habari(MAELEZO),
S.L.P.9142,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
JAMII YATAKIWA
KUJIHADHARI NA MATAPELI WANAOPITA
MAOFISINI KUWAHADAA VIONGOZI .
Serikali
inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania
kuwa hivi karibuni kumezuka kundi la Watu wadanganyifu ambao wamekuwa wakitumia
majina ya viongozi waandamizi wa serikali na Taasisi nyeti ikiwemo Usalama wa
Taifa kujipatia fedha kwa madai ya
kutumwa na viongozi hao.
Watu
hao wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwa maofisa mbalimbali wa
wizara, mashirika ya umma na Idara za Serikali zinazojitegemea kuomba pesa ili
wawafanye mipango ya kupandishwa vyeo.
Utapeli
huo umekuwepo nchini kwa kipindi kirefu sasa , ambapo watu huwapigia simu
viongozi wa Taasisi za fedha , Mifuko ya Taasisi za Jamii na watu binafisi
wakiomba fedha kwa madai ya kutumwa na viongozi waandamizi Serikalini wakati si
kweli.
Watu
hao wamekuwa wakiwatapeli maofisa mbalimbali kuwa wanaweza kuwafanyia mipango
ya kupandishwa vyeo endapo watawapatia kiasi cha fedha jambo ambalo halipo
katika taratibu za utumishi wa umma.
Utumishi
wa umma unazo taratibu zake za kuwapandisha vyeo watumishi wake kulingana na
sifa za kada zao na wala haiwezekani kwa viongozi waandamizi kuwachangisha
fedha kwa ajili ya kuwapandisha vyeo.
Serikali
inawataka wananchi kuwapuuza matapeli hao na watoe taarifa katika vyombo vya
dola na usalama mara wapatapo ujumbe wa aina hiyo ili hatua zichukuliwe dhidi yao.
IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI (MAELEZO) DAR ES SALAAM.
12.02.2013
No comments:
Post a Comment