Monday, February 11, 2013

PAPA BENEDICT ATANGAZA LEO KUJIUZULU

Pope Benedict
ROME, Italia
Pope Benedict ametangaza leo kuwa atajiuzulu cheo hicho cha juu katika Kanisa Katoliki duniani ifikapo Februari 28 huku akisema kwamba sababu ya kufanya hivyo ni uzee ambao sasa unamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

"Kwa sababu hiyo, na kwa sababu ya uzito wa suala lenyewe, na kwa uhuru kabisa, nathibitisha kwamba najiuzulu kuwa askofu wa Rome, mrithi wa Mtakatifu Peter," alisema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kutoka Vatican leo.

No comments:

Post a Comment