Monday, February 11, 2013

JAMAL MALINZI AFYEKWA UCHAGUZI TFF... SASA NJIA NYEUPE NYAMLANI KUMRITHI TENGA... MICHAEL WAMBURA PIA ACHINJIWA TENA BAHARINI...!

Jamal Malinzi

Athumani Nyamlani (wa pili kulia)

Michael Wambura

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Kagera na katibu mkuu wa zamani wa klabu ya Yanga, Jamal Malinzi ameambiwa kuwa hana uzoefu wa uongozi na hivyo kuondolewa katika kinyang'anyiro cha kuwania urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Taarifa iliyotolewa na TFF leo, imesema kuwa mgombea wa nafasi ya urais aliyepitishwa na hivyo kubaki katika mbio za kuwania kumrithi rais wa sasa, Leodger Tenga ni Athumani Nyamlani ambaye pingamizi alilowekewa limetupwa baada ya kuonekana kuwa utumishi wake serikalini haumzuii hata chembe kuongoza chombo hicho cha juu cha kusimamia mchezo wa soka nchini. Nyamlani ni makamu wa rais wa TFF anayemaliza muda wake.


Uamuzi wa kumuengua Malinzi umetolewa leo 
na Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya shirikisho hilo iliyokuwa ikipitia pingamizi mbalimbali ambapo wengine waliongeuliwa ni katibu mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT- sasa TFF), Michael Wambura ambaye alikuwa akiwania nafasi ya Makamu wa Rais na Ahmed Yahya aliyekuwa akiwania nafasi ya uenyekiti wa Bodi ya Ligi.

Malinzi aliwekewa pingamizi na baadaye kukatiwa rufaa na Agape Fue, aliyesema kuwa hana uzoefu. Uchaguzi wa TFF utafanyika Februari 24 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment