Sunday, February 3, 2013

MICHAEL OWEN KUADHIBIWA NA FA KWA KUMPIGA NGUMI ARTETA, ARSENAL IKISHINDA 1-0

Mikel Arteta wa Arsenal akijibizana na refa Chris Foy wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Stoke City baada ya Michael Owen (wa pili kulia) kumpiga Arteta kwenye Uwanja wa Emirates mjini London Februari 2, 2013.
Mikel Arteta wa Arsenal akijibizana na refa Chris Foy wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Stoke City baada ya Michael Owen (wa pili kulia) kumpiga Arteta kwenye Uwanja wa Emirates mjini London Februari 2, 2013.
Lukas Podolski akifunga kwa 'fri-kiki' wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Stoke City kwenye Uwanja wa Emirates mjini London Februari 2, 2013.

MICHAEL Owen huenda akakabiliwa na adhabu kutoka chama cha soka cha England (FA) kutokana na kumpiga Arteta ngumi Mikel Arteta wakati Stoke City ilipolala 1-0 kwa Arsenal.

Owen alionekana akimpiga kama ngumi kiungo wa Arsenal, Arteta mgongoni kuelekea mwishoni mwa mechi hiyo kwenye Uwanja wa Emirates.

Straika huyo hakuadhibiwa na refa lakini maafisa wa mamlaka ya soka watamchunguza baada ya kunaswa kwenye kamera.

Kocha wa Stoke, Tony Pulis alisema: "Arteta aliingia vibaya, lakini Michael hakupaswa kufanya vile."

Stoke ambao "walipaki basi" katika mechi nzima walitanguliwa kwa goli la dakika za lala salama kutokana na 'fri-kiki' iliyobadilishwa mwelekeo baada ya kugonga ukuta wa Stoke iliyopigwa na mtokea benchi Lukas Podolski.

"Kama Michael alifanya jambo lile wataangalia na kulishughulikia," aliongeza Pulis.

"Tutaona watakachosema. Mimi nitakuwa na upendeleo kwa sababu hii ni timu yangu ya soka."

No comments:

Post a Comment