Sunday, February 3, 2013

MGENI SISSOKO AIZAMISHA CHELSEA... DEMBA BA AVUNJIKA PUA

Gooooooo!..... Moussa Sissoko wa Newcastle United akifunga goli la ushindi dhidi ya Chelsea wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa St James' Park mjini Newcastle Februari 2, 2013.
Moussa Sissoko wa Newcastle United akifunga goli la ushindi dhidi ya Chelsea wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa St James' Park mjini Newcastle Februari 2, 2013.
Moussa Sissoko wa Newcastle United akishangilia kufunga goli la ushindi dhidi ya Chelsea wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa St James' Park mjini Newcastle Februari 2, 2013.

Kocha Alan Pardew wa Newcastle United akimpongeza Moussa Sissoko kwa kufunga goli la ushindi wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa St James' Park mjini Newcastle Februari 2, 2013.
Straika wa Chelsea, Demba Ba akipigwa teke la uso na beki wa Newcastle, Fabricio Coloccini wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa St James' Park mjini Newcastle Februari 2, 2013.
Straika wa Chelsea, Demba Ba akipigwa teke la uso na beki wa Newcastle, Fabricio Coloccini wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa St James' Park mjini Newcastle Februari 2, 2013.
Straika wa Chelsea, Demba Ba akipigwa teke la uso na beki wa Newcastle, Fabricio Coloccini wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa St James' Park mjini Newcastle Februari 2, 2013.
Straika wa Chelsea, Demba Ba akirejea uwanjani baada ya kutibiwa kufuatia kuvunjwa pua baada ya kupigwa teke la uso na beki wa Newcastle, Fabricio Coloccini wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa St James' Park mjini Newcastle Februari 2, 2013.

Jamaa hakuwa na kinyongo nao... Demba Ba akimsalimia kwa bashasha Yohan Cabaye kabla ya kuanza kwa mechi yao
MOUSSA Sissoko alifunga mara mbili katika mechi yake ya kwanza kwenye uwanja wa nyumbani wakati Newcastle walipozinduka kutoka nyuma na kushinda 3-2 dhidi ya Chelsea katika mechi iliyojaa utemi.

Straika wa zamani wa Newcastle, Demba Ba alikuwa na nafasi ya kwanza ya kufunga, lakini alipiga kichwa nje na kisha akatoka baada ya kugongwa na kiatu cha uso cha Fabricio Coloccini.

Dakika chache baada ya Demba Ba kutoka, Jonas Gutierrez aliwafungia Newcastle goli la kuongoza kwa kichwa lakini Chelsea walijibu vyema kwa goli la shuti la mbali kutoka kwa Frank Lampard na Juan Mata akatupia la pili kwa shuti la mkunjo wa ndizi.

Sissoko aliwasazisha katika dakika ya 68 na akafunga la ushindi katika dakika za majeruhi.

Kuingia kwa kiungo huyo Mfaransa, ambaye alijiunga na Newcastle Januari 25, ilikuwa ni nyongeza muhimu kwa mashabiki na alikuwa tishia wakati wote.

Kocha wa Newcastle, Alan Pardew alimuelezea nyota wake huyo mpya kuwa ndiye aliyeleta tofauti katika mechi yao waliyoshinda dhidi ya Aston Villa katikati ya wiki, na nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 alionyesha kuwa anatisha wakati aliposhirikiana vyema na Mfaransa mwenzake Yoan Gouffran aliyekuwa pia akicheza mechi yake ya kwanza nyumbani pamoja na Yohan Cabaye katika kutishia ngome ya wageni.

Ushindi wa pili mfululizo ambao ni kwa mara ya kwanza tangu Aprili mwaka jana umeiinua Newcastle pointi nane juu ya mstari wa kushuka daraja na kuashiria kwamba licha ya kumpoteza Ba aliyejiunga na mabingwa hao wa Ulaya mapema Januari, wanaweza kukwea juu zaidi kwenye msimamo.

Chelsea, licha ya kupambana vyema katika kipindi cha pili, walijikuta wakikumbana na kipigo chao cha kwanza tangu Desemba 1.

Kikosi cha Rafael Benitez sasa hakijashinda katika mechi nne zilizopita za michuano yote, na licha ya kwamba kulikuwa na matukio matamu, yakiwemo magoli ya kuvutia kutoka kwa Lampard na Mata, matokeo haya hayatarajiwi kumkubalisha Benitez kwa mashabiki wa Stamford Bridge.

Jioni ya Chelsea ilihitimishwa na kuumia kwa Ba, ambaye alikuwa na mechi ambayo atapenda kuisahau kwenye Uwanja wa St James' Park.

Msenegali huyo alizomewa tangu mwanzo na akaishia kuondoka uwanjani kabla ya mapumziko kwa kile kilichothibitishwa baadaye kwamba alivunjika pua baada ya kupigwa teke na Coloccini.

Tukio hilo lilikuja wakati Ba nusura awafungie Chelsea goli la kuongoza. Alipokea pasi ya Lampard na, wakati shuti lake la kwanza liliokolewa na Tim Krul, mpira ulimrudia na wakati akipiga kichwa kando kidogo ya lango, alikumbana na kiatu hicho cha Coloccini.

Ba alitibiwa kwa muda mrefu pembeni ya uwanja wakati damu ikimwagika kutoka puani mwake, ingawa refa Howard Webb hakumuadhibu beki huyo wa wenyeji.

NB: Frank Lampard, ambaye mkataba wake Chelsea unamalizika mwisho wa msimu huu, sasa amefunga magoli 10 au zaidi katika misimu 10 mfululizo ya Ligi Kuu ya England
.

No comments:

Post a Comment