Sunday, February 3, 2013

RONALDO AJIFUNGA... AIZAMISHA REAL MADRID 1-0 KWA TIMU YA MKIANI GRANADA

Ronaldo (7) akitupia goli katika nyavu zake mwenyewe wakati akijaribu kuokoa kona
Ronaldo akijilaumu baada ya kujifunga
Hoi.... wachezaji wa Real Madrid wakirudi kati baada ya Ronaldo kujifunga dhidi ya Granada usiku wa kuamkia leo


GOLI la kujifunga kutoka kwa Cristiano Ronaldo – ndio, umesoma sahihi, goli la kujifunga la Ronaldo – liliwapa Granada ushindi usiotarajiwa wa 1-0 dhidi ya Real Madrid, ambayo iliangukia katika siku zake mbaya za mwanzo wa msimu.

Kipigo hicho kinamaanisha kwamba kikosi cha kocha Jose Mourinho kinaendelea kubaki pointi 15 nyuma ya vinara Barcelona, ambao usiku wa leo watakuwa ugenini katika mechi ngumu dhidi ya Valencia.

Zikiwa zimekwenda dakika 21, mchezaji wa Granada, Nolito alipiga kona kutokea upande wa kushoto, ambayo Cristiano Ronaldo aliirukia kwa kichwa na kuutumbukiza mpira golini kwake mwenyewe.

Tono, kipa wa Granada, alilazimika kusubiri hadi dakika ya 57 kabla ya kupigwa shuti la kwanza la hatari la Real Madrid katika mechi nzima. Lilikuwa ni shuti la umbali mrefu kutoka kwa Cristiano Ronaldo, ambalo alilipangua na kuwa kona.

Kufikia wakati huo, Granada walikuwa wakicheza kwa kujiamini kupita kiasi nyuma, huku Real Madrid wakiwa hawawezi kucheza soka lolote la kupenya safu mbele.

Real Madrid waliongeza presha katika dakika za mwisho, na Tono alilazimika kuokoa tena kwa kujinyoosha kuokoa shuti la Callejon. Mpira uliorudi uliangukia kwa Benzema, lakini isivyotarajiwa alipiga nje wakati mashabiki wa Madrid wakiwa tayari wanashangilia goli la kusawazisha.

Ilikuwa ni mara ya kwanza katika maisha yake ya soka Cristiano Ronaldo kujifunga mwenyewe.

No comments:

Post a Comment