Alexis Sanchez wa Barcelona akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Getafe leo. |
Lionel Messi akichana msitu wa mabeki wa Getafe mchana wa leo. |
Alexis Sanchez wa Barcelona akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Getafe leo. |
MADRID, Hispania
LIONEL Messi alifunga goli lake la 35 la ligi msimu huu wakati timu iliyopumzisha wakali ya Barcelona ilipotoa kipigo cha 6-1 nyumbani dhidi ya Getafe na kuwafanya wapae kwa tofauti ya pointi 12 kileleni mwa msimamo wa La Liga leo.
Alexis Sanchez na David Villa walitumia vyema nafasi adimu ya kuanza katika kikosi cha kwanza kwa kufunga magoli huku Messi, Andres Iniesta, Cristian Tello na Gerard Pique nao kila moja akifunga wakati Barca ilipopata ushindi wa 20 katika mechi 23 za ligi msimu huu na kufikisha pointi 62.
Atletico Madrid walikuwa na pointi 50 katika nafasi ya pili kabla ya mechi yao ya jana saa 5:00 usiku dhidi ya Rayo Vallecano, pointi nne juu ya Real Madrid walio katika nafasi ya tatu, ambao waliwasambaratisha Sevilla 4-1 kwenye Uwanja wa Bernabeu Jumamosi.
Kocha wa muda wa Barca, Jordi Roura, ambaye anamshikia Tito Vilanova ambaye anauguza upasuaji wa koo, aliwapumzisha wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza katika mechi hiyo dhidi ya Getafe kwenye Uwanja wa Nou Camp, wakiwamo wachezaji watatu wa timu ya taifa ya Hispania, Pedro, Cesc Fabregas na Sergio Busquets.
Alexis alifunga katika dakika ya sita, Messi akafanya matokeo yawe 2-0 dakika saba baadaye na Villa alifunga la tatu kabla ya dakika ya 60 na kuifanya mechi iwe ngumu kwa Getafe, ambao wanashika nafasi ya 12 wakiwa na pointi 29.
Messi alikimbia mbele na kumtengea pasi mtokea benchi Tello aliyefunga na nne dakika 11 kabla ya mechi kumalizika kabla ya makosa ya beki wa kushoto Jordi Alba kumpa Alvaro Vazquez goli la kufutia machozi kwa wageni katika dakika ya 83.
Iniesta aliuwahi mpira uliozagaa na kufumua shuti la jirani na lango katika dakika ya 90 na kufunga la tano kabla ya Pique kukamilisha kipigo kizito katika dakika ya pili ya majeruhi akifunga katika goli tupu kufuatia pasi isiyo ya kichoyo ya Thiago Alcantara.
Wafungaji wanaoongoza katika Ligi Kuu ya Hispania baada ya mechi ya Barcelona mchana huu:
35 Lionel Messi (Barcelona)
24 Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
18 Radamel Falcao (Atletico Madrid)
12 Aduriz (Athletic Bilbao)
Ruben Castro (Real Betis)
11 Roberto Soldado (Valencia)
10 Piti (Rayo Vallecano)
Alvaro Negredo (Sevilla)
9 Carlos Vela (Real Sociedad)
Oscar (Real Valladolid)
Helder Postiga (Real Zaragoza)
8 Iago Aspas (Celta Vigo)
Riki (Deportivo Coruna)
Isco (Malaga)
Gonzalo Higuain (Real Madrid)
7 Pizzi (Deportivo Coruna)
Obafemi Martins (Levante)
Tomer Hemed (Real Mallorca)
Victor (Real Mallorca)
6 Cesc Fabregas (Barcelona)
Javier Saviola (Malaga)
Leonardo Carrilho Baptistao (Rayo Vallecano)
Joan Verdu (Espanyol)
Jorge Molina (Real Betis)
Karim Benzema (Real Madrid)
Manucho (Real Valladolid)
Matokeo na msimamo wa mechi za wikiendi za Ligi Kuu ya Hispania
Jumapili,Februari 10 Barcelona 6 Getafe 1 Jumamosi, Februari 9 Celta Vigo 0 Valencia 1 Deportivo Coruna 0 Granada CF 3 Levante 1 Malaga 2 Real Mallorca 1 Osasuna 1 Real Madrid 4 Sevilla 1 Msimamo P W D L F A Pts 1 Barcelona 23 20 2 1 78 26 62 2 Atletico Madrid 22 16 2 4 43 21 50 3 Real Madrid 23 14 4 5 58 22 46
4 Malaga 23 11 6 6 36 21 39
5 Valencia 23 11 4 8 32 35 37 6 Real Betis 22 11 2 9 31 34 35
7 Rayo Vallecano 22 11 1 10 31 38 34
8 Real Sociedad 22 9 6 7 35 28 33 9 Levante 23 10 3 10 29 35 33 10 Real Valladolid 22 8 5 9 32 29 29 11 Sevilla 23 8 5 10 30 34 29 12 Getafe 23 8 5 10 29 42 29 13 Granada CF 23 7 5 11 22 32 26 14 Athletic Bilbao 22 7 5 10 29 42 26 15 Espanyol 22 6 7 9 26 34 25 16 Real Zaragoza 22 7 3 12 22 31 24 17 Osasuna 23 5 7 11 19 27 22
18 Celta Vigo 23 5 5 13 21 28 20 19 Real Mallorca 23 4 6 13 23 43 18 20 Deportivo Coruna 23 3 7 13 27 51 16
No comments:
Post a Comment