Friday, February 8, 2013

MAVAZI YA UTATA MARUFUKU TUZO ZA GRAMMY JUMAPILI

Rihanna in The 54th Annual GRAMMY Awards - Show
KITUO cha televisheni cha CBS kimetoa taarifa wiki hii kikiwataka mastaa watakaohudhuria tamasha la 55 la tuzo za muziki za Grammy litakalofanyika keshokutwa kuvaa nguo zenye kuhifadhi maungo yao.

Katika barua pepe, kituo hicho cha televisheni kimewaeleza waalikwa kuhakikisha kwamba wanavaa mavazi ya kufunika maungo yao na kuepuka nguo za "utata" zikiwamo zinazoonyesha ndani.


Miongoni mwa mavazi ya utata katika historia ya Grammy ni gauni maarufu la Jennifer Lopez mwaka 2000; la Lea Michelle (2010), na la Toni Braxton la mwaka 2001.


Barua pepe kamili inasomeka:

"CBS inawashauri wasanii wote watakaotokea kwenye kamera kwamba tafadhali zingatia kanuni za mavazi za televisheni.

"Tafadhali hakikisha kwamba makalio na matiti ya wanawake yanazibwa vyema. Mavazi ya utata ni tatizo. Tafadhali epuka kuacha wazi ngozi ya chini muinuko wa makalio na inapoanzia njia ya mpasuko wa makalio chini ya mgongo. 


"Kuacha wazi maeneo ya chini ya matiti pia ni tatizo. Tafadhali epuka mavazi ya kitambaa kinachoonyesha ndani. Tafadhali hakikisha maungo yote ya siri yanafunikwa ili kusiwe na eneo la 'hatari' linaloanikwa. 

"Tafadhali epuka matangazo ya biashara ya bidhaa mbalimbali katika fulana. Maandishi ya lugha za kigeni yatahitaji kukaguliwa na kutambuliwa maana yake. MAVAZI YA KUJIANIKA HAYAKUBALIKI KURUSHWA HEWANI. Hii inawagusa pia mashabiki ambao watatokea kwenye kamera."

Jennifer Lopez (2000)Toni Braxton (2001)


Pink (2010)


Sheryl Crow (2002)


The "Lady Marmalade" Girls (2002)


Anne V (2012)


Rihanna (2011)


Celine Dion (1993)


M.I.A. (2009)


Margaret Cho (2004)


Christina Aguilera (2004)


Rihanna (2011)
The 53rd Annual GRAMMY Awards - Arrivals

Lady Gaga (2010)
52nd Annual GRAMMY Awards - Arrivals

Destiny's Child (2001)


Christina Augilera (2001)


Britney Spears (2000)


Lil Kim (2004)


Fergie (2004)


Katy Perry (2009)
Katy+Perry in 51st Annual Grammy Awards - Show

Bai Ling (2008)


Ciara (2011)
Ciara in 53rd Annual GRAMMY Awards

(Photos: Getty Images | CBS)

No comments:

Post a Comment