Friday, February 8, 2013

VALENCIA ASHINDA VITA YA KWANZA DHIDI YA RONALDO

Antonio Valencia (kushoto) wa timu ya taifa ya Ecuador akiwania mpira dhidi ya Cristiano Ronaldo wa Ureno wakati wa mechi yao ya kirafiki ya kimataifa juzi Jumatano. Ecuador walishinda 3-2. 

ECUADOR walisafiri kwenda Ureno na kuwapa wenyeji kipigo kisichotarajiwa cha 3-2.

Ushirikiano wa Antonio Valencia na Felipe Caicedo ulitosha kulifunika goli gali lililofungwa na nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo, na kumhakikishia kwamba hana cha ziada cha kufurahia katika siku yake ya kuzaliwa.

Valencia, kiungo wa Manchester United ambaye alifunga goli moja kati ya matatu ya Ecuador, amemuangusha Cristiano katika mpambano wa kwanza baina yao wakiwa na timu zao za taifa.

Wawili hao watakutana tena tena Jumatano, katika mechi ya hatua ya 16-Bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wakati klabu zao za Real Madrid na Manchester United zitakapochuana kuwania kutinga robo fainali.

No comments:

Post a Comment