Thursday, February 7, 2013

MESSI ASAINI MKATABA MPYA BARCELONA HADI 2018

Lionel Messi akimwaga wino

MWANASOKA Bora wa Dunia Lionel Messi amesaini mkataba mpya na Barcelona unaomfunga hadi Juni 30 2018, vinara hao wa La Liga wamesema leo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amesaini dili hilo aliloliafiki Desemba, ambalo linajumuisha kuongezwa miaka miwili katika mkataba wake wa awali na hivyo kubaki hapo hadi akiwa na umri wa miaka 31.

Nahodha huyo wa timu ya taifa Argentina alijiunga na timu ya vijana ya Barcelona akiwa na umri wa miaka 13 na alichezea timu ya wakubwa kwa mata ya kwanza wakati akiwa na miaka 16.

Messi ndiye anayeshikilia rekodi ya kuifungia timu hiyo magoli mengi zaidi ya wakati wote, na amekuwa mfungaji bora wa Ligi ya Klabu Bingwa katika misimu minne mfululizo iliyopita na alimaliza kalenda ya mwaka 2012 akiweka rekodi ya kufunga magoli 91 kwa klabu na nchi yake.

No comments:

Post a Comment