Monday, February 11, 2013

MAN UTD POINTI 12 JUU YA MAN CITY... CHEZEA VAN MAGOLI WEWE!!?

Ryan Giggs of Manchester United scores the opening goal during the Barclays Premier League match between Manchester United and Everton at Old Trafford on February 10, 2013 in Manchester, England.
True Legend... Kaka wewe ni gwiji wa kweli... Wachezaji wa Manchester United wakimpongeza Ryan Giggs kwa kufunga goli. Giggs amecheza misimu yote 23 ya Ligi Kuu ya England tangu ligi hiyo ilipobadilishwa kutoka kuitwa Ligi Daraja la Kwanza na goli hilo limemaanisha kwamba amefunga katika misimu yote ya ligi hiyo.
Van Magoli akimfunga Tim Howard wa Everton goli la pili

Tulia wewe... Van Magoli akitupia goli lake huku kipa Tim Howard akiwa hana la kufanya
Gooooo.

Van Magoli akishangilia goli lake dhidi ya Everton

RVP akishangilia goli lake dhidi ya Everton
Goli la ngapi hili mnisaidie kuhesabu....

Chezea mimi wewe?.... RVP akishangilia goli lake dhidi ya Everton

MANCHESTER United waliongeza tofauti ya pointi kileleni mwa msimamo kufikia pointi 12 kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Everton kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Kikosi cha Sir Alex Ferguson walitumia vyema makosa ya mabingwa Manchester City kufungwa 3-1 dhidi ya Southampton Jumamosi na kuweka tofauti kubwa ya pointi wakati wakisaka ubingwa wao wa 20 wa Ligi Kuu ya England.

United hawakuweka akili nyingi katika kuwiwaza mechi yao ya Jumatano ya hatua ya 16-Bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidio ya Real Madrid kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu kwani walishusha kikosi kamili kwa ajili ya ushindi huo mwingine muhimu.

Kocha wa Real, Jose Mourinho alishuhudia mechi kutokea kwenye eneo la wakurugenzi la jukwaa la Old Trafford wakati Ryan Giggs akifunga goli katika msimu wake wa 23 mfululizo kwenye ligi kuu na kuipa United goli la mapema la kuongoza kabla ya Robin van Persie hajaongeza jingine ambalo lilikuwa ni la 23 kwake msimu huu kabla ya mapumziko.

Everton hawakuonekana kama wangeweza kuzinduka kama walivyofanya msimu uliopita walipoibuka kutoka 2-0 nyuma na kulazimisha sare ya 4-4 kwenye Uwanja wa Old Trafford. Huku kulikuwa kuzinduka ambako kuliathiri kampeni za kuwania taji za United lakini mara hii hawakuonyesha kuwa wanaweza kurudia jambo hilo.

No comments:

Post a Comment