Saturday, January 26, 2013

ZAHA ATISHIA 'MAISHA' YA VALENCIA MAN UTD

Wilfried Zaha
Wilfried Zaha

Antonio Valencia

Wilfried Zaha

KUSAJILIWA kwa Wilfried Zaha kumegeuka kuwa moto kwa Antonio Valencia klabuni  Manchester United.

United hata hivyo hawatamkaribisha Zaha kutoka Crystal Palace hadi mwisho wa msimu, lakini kuwasili kwake kutaongeza presja kwa winga mwenzake Valencia.

Gazeti la Manchester Evening News limesema kuwa kocha wa Man United, Sir Alex Ferguson daima amekuwa akimfagilia Valencia na alimkabidhi jezi yenye heshima ya Na.7 Juni mwaka jana.

Lakini nyota huyo wa Ecuador ameshuka kiwango katika wiki za karibuni na hajaanza kata mechi moja ya Ligi Kuu tangu mwaka huu uianze.

Aliachwa nje ya kikosi kilichoanza katika mechi mbili kubwa zaidi za Man United mwezi huu dhidi ya Liverpool na Tottenham – na alileta mchango mdogo wakati alipoingia akitokea benchi.

Zaha anatarajiwa kuleta ushindani mkubwa zaidi kwa winga huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye namba yake ya kudumu katika kikosi cha kwanza haiko salama tena sasa kama ilivyokuwa awali.

Yosso mwenye kipaji Zaha amekamilisha kujiunga na Man United kwa ada ya uhamisho inayotajwa kuwa ni paundi milioni 15 akitokea Crystal Palace lakini ataendelea kuichezea klabu hiyo kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.

No comments:

Post a Comment