Saturday, January 26, 2013

ODEMWINGIE AWASILISHA BARUA YA KUOMBA KUONDOKA WEST BROM AENDE KWENYE "MAHELA" QPR

Peter Odemwingie

STRAIKA wa West Brom, Peter Odemwingie amewasilisha barua ya kuomba kuhama klabu hiyo.

Amedhamiria kuzungumza na kocha wa QPR, Harry Redknapp, ambaye yuko tayari kuongeza ofa aliyowasilisha awali ya paundi milioni 3 — kwa paundi milioni 1 zaidi.

Lakini West Brom Albion wamekataa ombi hilo la Odemwingie na kusema kwamba hakuna mchezaji wao yeyote "jembe" atakayeuzwa.

Odemwingie amebakiza miezi 18 katika mkataba wake wa sasa na Albion.

Mkurugenzi wa michezo na ufundi wa West Brom, Richard Garlick amesema: "Hatujitaji kumuuza mchezaji wetu tegemeo yeyote. Tunataka kukiweka pamoja kikosi chetu.”

No comments:

Post a Comment