Saturday, January 26, 2013

KAMPUNI YA NIKE YAISUKUMA PSG IMNUNUE ROONEY


Wayne Rooney

PSG wanajiandaa kutuma maombi ya kustusha mwisho wa msimu ya kutaka kumsajili straika wa Manchester United, Wayne Rooney - maombi ambayo yanapata sapoti kutoka kwa kapuni ya Nike.

Gazeti la Daily Mail limesema kuwa wasambazaji wa jezi za PSG, Nike, wanataka kuhakikisha kwamba klabu hiyo ya Ufaransa inalipa kiasi chochote kitakachohitajika ili kumsajili straika wa Manchester United, Rooney.

Straika huyo wa timu ya taifa ya England hakuwa na furaha kutokana na kuachwa nje ya kikosi cha United kilichoivaa Tottenham wiki iliyopita na Nike wanataka kumpata Rooney, ambaye jezi yake ya Man United ndiyo inayouzwa kuliko jezi yoyote kwenye Ligi Kuu ya England.

No comments:

Post a Comment