Wednesday, January 23, 2013

YANGA-MBIWA ASAINI MIAKA 5 NEWCASTLE

Mapou Yanga-Mbiwa

NEWCASTLE United wamemsajili beki Mapou Yanga-Mbiwa kutoka katika klabu ya Ufaransa ya Montpellier kwa ada isiyotajwa, inayoaminika kuwa ni paundi milioni 6.7.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 amesaini mkataba wa miaka mitano na nusu klabuni St James' Park.

Na mshambuliaji wa Bordeaux, Yoan Gouffran amebainisha kwamba pia anajiandaa kutua Newcastle leo.

Aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter:  "Kesho (leo) nitakuwa mchezaji mpya wa Newcastle na najivunia. Shukrani kwa kila mmoja."

Newcastle, ambao tayari wamemsajili beki wa kulia wa Ufaransa, Mathieu Debuchy katika kipindi hiki cha usajili cha Januari, pia wanakaribia kumsajili beki Massadio Haidara kutoka klabu ya Nancy ya Ufaransa pia.

Yanga-Mbiwa alikuwa nahodha wa Montpellier wakati wakitwaa taji lao la kwanza la Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1, msimu uliopita aliichezea klabu hiyo zaidi ya mechi 200.

"Ni heshima kutua katika klabu ya Newcastle United na kuwa na nafasi ya kucheza katika Ligi Kuu ya England," alisema.

No comments:

Post a Comment