Wednesday, January 23, 2013

RONALDO ALIKATALIWA BARCELONA

Si mlinikataa.... Ronaldo wa Real Madrid akishangilia baada ya kuwafunga Barcelona. Ronaldo anashikilia rekodi ya kufunga magoli katika mechi sita mfululizo za Classico dhidi ya Barcelona.
RAIS wa zamani wa Barcelona, Joan Laporta amebainisha kwamba walikataa fursa ya kumsajili Cristiano Ronaldo.

Laporta amesema nyota huyo wa Real Madrid alitolewa ofa kwa Barca na wakala Jorge Mendes wakati akiichezea Sporting Lisbon - tena kwa pesa ndogo zaidi ya ambayo Manchester United waliitumia kumsajili.

"Mendes alimleta kwetu, tena kwa bei poa zaidi ya aliyonunuliwa kwenda Manchester.

"Tungeweza kumnunua, lakini kwa wakati ule tulikuwa tunadhibiti matumizi ya fedha baada ya kuwa tumeshawanunua Ronaldinho, Marquez na Quaresma."


Tangu atue Real Madrid akitokea Manchester United misimu mitatu na nusu iliyopita, Cristiano Ronaldo ameweka rekodi mpya ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika mechi sita mfululizo za Classico dhidi ya Barcelona.

No comments:

Post a Comment