Wednesday, January 23, 2013

SHAKIRA AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME, ASAJILIWA BARCA

Shakira akiwa na Gerard Pique
Shakira akiwa na Gerard Pique
Shakira akiwa na Gerard Pique


SHAKIRA amejifungua mtoto wa kiume jana usiku.

Yeye na patna wake nyota wa soka wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Gerard Pique, walitoa taarifa hizop mpya kwenye tovuti ya muimbaji huyo kufuatia ujumbe uliosema:

"Tuna furaha kutangaza kuzaliwa kwa Milan Piqué Mebarak, mtoto wa Shakira Mebarak na Gerard Piqué, aliyezaliwa Januari 22 saa 9:36 usiku, mjini Barcelona, Hispania.

Jina Milan (linalotamkwa MEE-lahn), linamaanisha "mpendwa, mpenzi, mchapakazi, mwenye usongo.

Kama baba yake, mtoto Milan amekuwa memba wa klabu ya FC Barcelona wakati akizaliwa.

Hospitali aliyozaliwa ilithibitisha kwamba mtoto huyo wa kwanza wa wapendanao hao alizaliwa akiwa na uzito wa Kg 2.7, na kwamba mama na mwanae wote wako katika afya njema.

No comments:

Post a Comment