Friday, January 4, 2013

WENGER: MASHABIKI WANATAKA TUMSAJILI MESSI MPYA

Kocha Arsene Wenger
Lionel Messi mwenyewe wa Barcelona

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema soka la uhamisho limekuwa gumu sana katika miaka ya karibuni.

Akibainisha kwamba kazi imekuwa ngumu kuliko ilivyokuwa wakati akiwasili Arsenal Septemba 1996, amekiri kwamba presha iliyopo daima ni kutakiwa "kumtafuta Lionel Messi mpya".

Wenger alisema: "Watu wanataka kumuona Lionel Messi mpya - hawataki kuona mtu mwenye kipaji kinachokua. Jina la mchezaji linawapa watu matumaini, lakini wakiwa hawajawahi kumsikia wanakuwa wazito kumkubali.

"Kazi ni ngumu zaidi kwetu hivi sasa. Ushindani ni mkubwa. Tunajaribu kusaka vipaji kwingineko kwa sababu hapa England tumebanwa kiasi. Soko jipa ya vipaji linalovutia ni Japan - kuna ushindani.

"Nchi ambayo tulikuwa tunamudu zaidi ushindani ilikuwa ni Ufaransa, lakini siku hizi wanazalisha wachezaji wa kiwango cha juu wachache, kuliko ilivyokuwa, tuseme miaka 15 iliyipota.

"Nchi zilizoibukia kutoa wachezaji bora ni Ujerumani na Hispania - wameshika usukani kutoka kwa Ufaransa na wana wachezaji vijana wakali wengi sana."

No comments:

Post a Comment