Friday, January 4, 2013

VAN DER VAART AKIRI KUMDUNDA MKEWE

Van der Vaart akiwa na mkewe Sylvie
Mke wa Van der Vaart, Sylvie
Sylvie Van der Vaart

Van der Vaart

KIUNGO wa Uholanzi, Rafael Van der Vaart, amekiri kumdunda mkewe mwanamitindo Sylvie Van der Vaart katika sherehe ya mkesha wa Mwaka Mpya.

"Kilikiwa ni kitendo cha kipuuzi sana kutoka kwangu. Mimi ni mjinga. Samahani  sana. Haikupaswa kutokea," kiungo huyo wa Hamburg aliliambia jarida la 'Bild' la Ujerumani.

Kufuatia tukio hilo, wanandoa hao wametangaza kwamba wataachana, kwa mujibu wa 'Bild'. Tukio hilo lilitokea katika sherehe ya faragha mjini Hamburg. Kabla ya ugomvi huo, wawili hao walipozi kwa picha pamoja wakionekana wanapendana na wenye furaha.

Hata hivyo, muda mfupi baadaye wawili hao waliingia katika majibizano makali ambayo yalifikia wakati kiungo huyo kumpiga mkewe, pigo lililomfanya aanguke sakafuni. Ingawa mwanamitindo huyo alidai hadharani kwamba amemsamehe mumewe, imebainika kwamba wameamua kila mmoja kushika hamsini zake.

No comments:

Post a Comment