Friday, January 4, 2013

RIHANNA, CHRIS BROWN WALIAMKA PAMOJA MWAKA MPYA?

Rihanna anaonekana akiwa amelala katika picha aliyoituma kwenye ukurasa wake wa Twitter asubuhi ya Mwaka Mpya akiwa amejifunika shuka la madoa-doa
Picha iliyotumwa na Chris Brown kwenye ukurasa wake wa Twitter ikionyesha miguu yake tu, lakini pembeni likionekana shuka kama alilojifunika Rihanna katika picha aliyoituma muda huo huo kwenye Twitter
Tupige picha shosti nakukubali sana... Shabiki akipiga picha na Rihanna baada ya kumuona mtaani akitokea dukani akijiandaa kuingia kwenye gari linaloendeshwa na Chris Brown mjini Los Angeles, California Januari 2, 2013. Wapendanao hao walikuwa pamoja pia Januari 1, 2013.
Tabasamu basi kidogo jamani... Shabiki akiendelea kupiga picha na Rihanna
Jamani nimefurahi kukuona 'live', kila siku nakuona kwenye video tu... Shabiki akiendelea kupiga picha na Rihanna.
Ngoja niwapige kwa huku nikahadithie kuwa nimewakuta mko pamoja.....
Yeees hilo ni bonge la pozi.... shabiki akiwapiga picha Rihanna na Chris Brown, huku Chris Brown (kwenye steringi kulia) akipozi kwa kuweka ishara ya vidole viwili kama vilivyomponza mwanajeshi wa Mbunge Godbless Lema

RIHANNA na Chris Brown huenda walilala pamoja siku ya Mwaka Mpya baada ya asubuhi yake wote kutuma picha mbili tofauti katika mtandao wa Twitter zinazoonyesha mazingira yanayofanana.

Ingawa picha hizo haziwaonyeshi wakiwa pamoja, lakini shuka alilojifunika Rihanna linaonekana pia katika picha iliyotumwa na Chris.

Nyota wa kibao cha 'Diamonds' Rihanna alituma picha inayomuonyesha akiwa amejifunika shuka akionyesha sura yake na kidole chake chenye tattoo isomekayo 'love', akiambatanisha na salamu "Asubuhi njema! Bado sijalala (kicheko) #hello2013".

Brown pia alituma picha aliyojipiga akiwa kitandani lakini alionyesha miguu yake tu na pembeni akionekana kama mtu kajifunika shuka lile lile alilojifunika Rihanna katika picha yake. Muda mfupi baadaye akaiondoa picha hiyo.

No comments:

Post a Comment