Wednesday, January 2, 2013

STURRIDGE ATIMKA CHELSEA... ATUA LIVERPOOL LEO

Daniel Sturridge
LONDON, England
Straika wa kimataifa wa England, Daniel Sturridge ametua rasmi Liverpool akitokea kwa mabingwa wa Ulaya, Chelsea kwa ada ya uhamisho isiyotajwa.

"Nimefurahi kuwa hapa (Liverpool)," straika huyo mwenye miaka 23 ameiambia tovuti ya klabu yake leo (www.liverpoolfc.com).

"(Kocha) Brendan Rodgers amesema ameniona tayari nikiwa hapa kitambo na mimi pia nimejiona hapa kwa muda mrefu. Sijasaini hapa kucheza kwa miaka kadhaa na kuondoka."

Liverpool haikutaja kipindi atakachokaa Sturridge lakini imesema kuwa amesaini kuichezea kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment