Thursday, January 3, 2013

KIBABU CHA PLAYBOY CHAOA BINTI MDOGO KWAKE KWA MIAKA 60

Mmiliki wa Playboy, Hugh Hefner (86) akiwa na mkewe Crystal Harris (26)
Bw. na Bi. Hugh Hefner wakiwa altareni
Hef akiwa na rafikize wa kike aliodumu nao kwa muda mrefu Holly Madison, Kendra Wilkinson, Bridget Marquardtna
Jumba la Playboy


MMILIKI wa jarida la Playboy,  Hugh Hefner (86) na mchumba wake mwanamitindo, Crystal Harris (26) wamefunga ndoa katika sherehe iliyofanyika katika mkesha wa Mwaka Mpya katika jumba la Playboy Mansion mjini Los Angeles, vyanzo kutoka ndani ya jumba hilo maarufu wameliambia gazeti la Us Weekly.

Awali baada ya kutangaza uchumba kwa Hefner Desemba 2010, mwanadada Harris alifuta ndoa yao iliyopangwa kufanyika Juni 2011 siku chache kabla ya harusi.

Mwaka mmoja baadaye, Harris amethibitisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba amemaliza tofauti zake na mpenziwe huyo wa zamani. Wawili waliimarisha mipango yao ya kufunga ndoa kwa mara nyingine mapema Desemba wakati walipopata leseni ya ndoa mjini Beverly Hills na Harris aliyejawa na furaha alijivunia kuionyesha pete yake ya uchumba. (Aliiuza katika mnada pete yake ya awali -- iliyokuwa na thamani ya dola 90,000! -- katika mnada wa NYC Oktoba 2011.)

Akizungumzia sababu ya kufanya sherehe hiyo ya pili kuwa ya siri, Harris -- ambaye hivi karibuni alifungua mtandao wake binafsi wa mavazi ya ndani uitwao Femme Fatale mjini California -- alisema anataka muunganiko wao wa sasa ume ni madhubuti zaidi.

"Ndoa yetu ilipovunjika kwa mara ya kwanza ilikuwa sababu ni mimi. Nilihitaji kukaa nje ya ndoa na kuona hali ya mambo. Katika kipindi nilichokuwa kule nilibaini kwamba mimi ninatakiwa kuwa hapa na Hef," Harris aliliambia gazeti la Us Weekly. "Mahusiano yetu ni mazuri kuliko yalivyokuwa zamani. Nina furaha na Hef ana furaha pia. Sote tumepagawa."

Harris awali alikuwa ni mmoja wa vimwana wa kipindi cha televisheni cha "Girls Next Door" kinachoonyesha maisha halisi yanayoendelea ndani ya Jumba la Playboy ambapo babu huyo anaishi maisha ya ajabu ya kuwa na wanawake saba, ambao baadaye walipungua na kubaki watatu, ambao wanapendana na kufanya kazi pamoja na anatoka nao kwa pamoja kwenda nao kwenye dhifa mbalimbali, huku wote wakiwa ni "mademu" wake tu.

Ndoa na Harris ni ya tatu kwa tajiri huyo anayemiliki jarida la Playboy, klabu za usiku na mtandao wa filamu za watu wazima. Hef aliwahi kumuoa Mildred Williams mwaka 1949 na wapakata watoto wawili -- Christie na David -- kabla ya kuachana mwaka 1959. Akamuoa Kimberley Conrad, mama wa watoto wake wawili Marston na Cooper, mwaka 1989 na wakatalikiana mwaka 2009 baada ya miaka 11 ya kutengana. Rafikize wa kike wa zamani ni pamoja na Holly Madison, Kendra Wilkinson, Bridget Marquardtna Brande Roderick.

Babu huyo anasemekana "ametembea" na wanawake zaidi ya 1,000.


No comments:

Post a Comment