Wednesday, January 2, 2013

SAJUKI SASA KUZIKWA JIJINI DAR ES SALAAM KESHOKUTWA IJUMAA BAADA YA SWALA SAA 7:00 MCHANA... NI KWENYE MAKABURI YA KISUTU BAADA YA BABA YAKE MZEE KILOWOKO KUKUBALI MAOMBI YA MASWAHIBA ZAKE KIBAO DAR WALIOTAKA KUSHIRIKI MAZISHI YAKE MWANZO-MWISHO...!

Sajuki akichapa mzigo enzi za uhai wake
Sajuki na mkewe Wastara enzi za uhai wake
Baba yake Sajuki... Mzee Kilowoko akiwasiliana na ndugu na jamaa kwa simu wakati akiwa kwenye msiba wa mwanawe, Tabata jijini Dar es Salaam leo Januari 2, 2013. Familia imeamua Sajuki azikwe makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam keshikutwa Ijumaa, Januari 4, 2013.

Wasanii wa vichekesho, Mtanga (kushoto) na Kiwewe (aliyejishika goti) wakiwa na waombolezaji wengine katika msiba wa Sajuki leo Januari 2, 2013.

Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Sajuki leo Januari 2, 2013.
Tutakukumbuka milele Sajuki... msanii nyota wa filamu za Kibongo, Suzan Lewis 'Natasha' akiwa kwenye msiba wa Sajuki mapema leo kushiriki maandalizi ya shughuli za mazishi, eneo la Tabata jijini Dar es Salaam leo Janauri 2, 2013..
Baadhi ya waombolezaji wa msiba wa Sajuki waliofika mapema Tabta, leo Januari 2, 2012. 

Piga pale...! Sajuki (kulia) akiwa katika maandalizi ya filamu yake mojawapo kali wakati wa enzi za uhai wake.


Waombolezaji wakiwa na majozni tele katika msiba wa Sajuki, Tabata jijini Dar es Salaam leo Januari 2, 2013.
Hatimaye ule utata kuhusiana na mahala pa kumzika msanii Juma Kilowoko 'Sajuki' umepatiwa jibu baada ya baba yake kukubali kuwa azikwe jijini Dar es Salaam.

Kutokana na uamuzi huo, sasa msanii huyo aliyekuwa nyota na kipenzi cha wengi enzi za uhai wake atazikwa keshokutwa
(Januari 4, 2013) saa 7:00 mchana baada ya swala ya Ijumaa kwenye makaburi ya Kisutu.

Awali, baba wa msanii huyo alitaka mwanawe akazikwe kwao mkoani Songea. Hata hivyo, baada ya kuketi na kujadili kwa kina na familia yake, akaamua kutangaza kuwa mwanawe huyo kipenzi atazikwa jijini Dar es Salaam ili kutoa nafasi kwa rafiki zake wengi aliokuwa akishirikiana nao katika kazi zake za kila siku za kisanii kupata nafasi ya kushiriki mazishi yake.

Mzee Kilowoko ametoa msimamo huo mpya leo hoo hii, ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kutangaza awali kuwa mwanawe atakwenda kuzikwa Songea.

Sajuki amefariki leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi na kupumua kwa msaada wa mashine kabla ya kuaga dunia mishale ya saa 1:00 asubuhi.Mashabiki wa filamu za Kibongo nchini watamkumbuka marehemu kwa filamu zake kama 'Round', 'Shetani wa Pesa', 'Hero of the Church', 'Vita' na 'Briefcase, 'Revenge', 'Dhambi', 'Mboni Yangu', 'Two Brothers', na'Behind the Scene'.

Sajuki alizaliwa mwaka 1986 Songea mkoani Ruvuma, ameacha mke na mtoto mmoja.

No comments:

Post a Comment