Wednesday, January 2, 2013

REAL MADRID MWAKA WA SHETANI... PEPE APASULIWA ENKA... AUNGANA 'WODI YA WAGONJWA' NA KINA MARCELO NA COENTRAIO ..RAMOS NAYE NJE J'PLI WAKIIVAA SOCIEDAD!

Pepe (kushoto) akiwa kazini. Hapa ni katika mechi yao Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya iliyomalizika kwa sare dhidi ya 2-2 dhidi ya Borussia Dortmund.

MADRID, Hispania
BEKI 'jembe' wa kati wa Real Madrid, Pepe amefanyiwa upasuaji wa enka ya mguu wa kulia leo Jumatano (Januari 2, 2013), mabingwa hao wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania, hivyo kumuongezea tatizo kocha Jose Mourinho katika kuteua mabeki kwenye kikosi chake cha kwanza.

"Baada ya kujisikia maumivu katika enka ya mguu wake wa kulia na kufanyiwa vipimo vya afya, mchezaji wa Real Madrid, Pepe alifanyiwa upasuaji wa leo asubuhi mjiniPorto," klabu hiyo ilisema kupitia tovuti yake (www.realmadrid.com).

Haikuelezwa hata hivyo ni kwa muda gani beki huyo wa kimataifa wa Ureno atakuwa nje lakini vyombo vya habari vya Hispania vimeripoti kuwa atakosekana kwa mwezi mmoja.

Huu ni kama mwaka wa mikosi kwa safu ya mabeki wa Real Madrid kwani katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakicheza pia bila mabeki wao nyota wa kushoto, Fabio Coentrao na Marcelo ambao wote wanauguza majeraja.

Pacha wa Pepe wa kila siku katika eneo la beki ya kati, Sergio Ramos, pia atakosekana katika mechi yao ya nyumbani Jumapili dhidi ya Real Sociedad akitumikia adhabu huku yosso wa Ufaransa, Raphael Varane akitarajiwa ndiye acheze kwa pamoja na beki asiyechezeshwa sana, Ricardo Carvalho wakati Real Madrid itakapokuwa ikisaka uwezekano wa kurejea katika makali yake kwenye La Liga kufuatia mwanzo mbaya.

Hadi sasa wako katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya mechi 17, wakiachwa kwa pointi saba na Atletico Madrid wanaoshika nafasi ya pili na pia pointi 16 na vinara wa ligi hiyo ambao hawajafungwa hadi sasa, klabu ya Barcelona.

No comments:

Post a Comment