Monday, January 21, 2013

RONALDO AMWAMBIA MOURINHO: NIMETOA MAISHA YANGU KWA AJILI YAKO, HUPASWI KUNISHUTUMU

Ronaldo


RIPOTI zaidi kuhusu majibizano baina ya kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho na Cristiano Ronaldo zimezidi kumiminika. 


Wawili hao walitofautiana wakati wa ushindi wa mechi ya Kombe la Mfalme dhidi ya Valencia. 

Mourinho alidaiwa kumwambia Ronaldo: "Katika dakika 15 za mwisho ulijificha, Cris. 

"Joao Pereira alikuwa anatusumbua sana kwenye wingi wa kulia. Unajua mechi hizi za mtoano goli moja ni muhimu sana. Unatakiwa upambane hadi mwisho." 

Baada ya kauli hiyo ya Mourinho, Ronaldo alijibu: "Nimejitoa maisha yangu kwa ajili yako, huna haki ya kunishutumu."

Picha za video zilimuonyesha Mourinho akimbwatukia Ronaldo baada ya nyota huyo kukosa goli.

  

No comments:

Post a Comment