Monday, January 21, 2013

VAN MAGOLI: NILIKUWA SAHIHI KUONDOKA ARSENAL

Robin van Magoli
 STRAIKA wa Manchester United, Robin van Persie amesema kipindi kilichopita cha usajili kilikuwa sahihi kwake kuondoka Arsenal.

Van Persie anakumbuka mafanikio yake Arsenal, ambako alifunga magoli 132 katika mechi 277, lakini anakubali kwamba ulikuwa ni wakati mwafaka kuondoka na kutua Man U kwa ajili ya kupigania mataji.

Alisema: "Muda uliwadia tu, nadhani Sir Alex alisema hilo wiki iliyopita, alisema 'Robin yuko hapa katika muda sahihi, wakati sahihi na klabu sahihi.' Nami naona hivyo.

"Naona kabisa kwamba huu ni wakati sahihi kwangu kuwapo hapa. Sidhani kama ilikuwa sahihi kwangu kuja hapa mapema zaidi. Nadhani mambo yote huenda hivi kwa sababu maalum.

"Kwa mfano, nilipoongeza mkataba wangu Arsenal miaka kadhaa iliyopita niliona kwamba lile lilikuwa ni jambo sahihi, kubaki na kucheza kwa sababu nilikuwa sijamaliza kazi yangu pale.

"Hivi sasa, tangu kipindi kilichopita cha usajili, nimekuwa na hisia kubwa ya kupigania mataji, na hii ndiyo changamoto kubwa kwangu hivi sasa."

No comments:

Post a Comment