Monday, January 21, 2013

ARSENAL WATAKA KUMSAJILI VICTOR WANYAMA

Victor Wanyama wa Celtic akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Barcelona wakati wa mechi yao ya Kundi G la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Celtic Park mjini Glasgow, Scotland November 7, 2012.
ARSENAL wamejumuika katika mbio za kuwania kumsajili kiungo wa Celtic, Victor Wanyama.
 

Kiungo huyo Mkenya amekataa mazungumzo ya mkataba mpya na Celtic.

Gazeti la Daily Mail la Uingereza limeripoti leo kuwa Arsenal imejumuika pamoja na Fulham katika mbio za kuwania kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 21.

Kiungo huyo mwenye mwili mkubwa anaonekana kufunika umaarufu wa kaka yake McDonaldo Mariga aliyeibuka kuwa nyota wa kwanza wa Afrika Mashariki Kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, wakati alipofunga goli dhidi ya Barcelona katika mechi yao ya hatua ya makundi kwenye Uwanja wa Celtic Park mjini Glasgow, Scotland November 7, 2012.

No comments:

Post a Comment