Wednesday, January 23, 2013

PUYOL AONGEZA MKATABA BARCA HADI 2016

Carles Puyol

NAHODHA wa Barcelona, Carles Puyol amesaini mkataba mpya utakaomweka hadi mwaka 2016.

Puyol alimwaga wino katika hafla iliyofanyika juzi.

Alisema: "Mtazamo wangu ilikuwa ni kuendelea kucheza hapa, nataka kubaki hapa kwa miaka mingi iwezekanavyo. Nashukuru kwa juhudi zilizofanywa na klabu, kusaini mkataba huu ni muhimu sana, lakini lililo muhimu zaidi ni kuumaliza."

Puyol pia alizungumzia muda wake mrefu kwenye soka:

"Kubaki fiti ni jambo muhimu sana nafahamu kwamba natakiwa kujilinda ndani na nje ya uwanja. Hicho ndicho nitakachojaribu kukifanya.

"Natakiwa kulifanya hili msimu mmoja hadi mwingine, lakini matumaini yangu ni kuendelea kucheza soka hadi nikiwa na miaka 40."

No comments:

Post a Comment