Tuesday, January 8, 2013

OMAR OMAR WA MCHIRIKU AFARIKI DUNIA


NYOTA wa muziki wa Mchiriku, Omar Omar amefariki dunia leo.

Kwa mujibu wa mtangazaji Gerald Hando wa kipindi cha Power Breakfast cha Radio Clouds FM, muimbaji huyo amefariki leo kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu, siku moja tu baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Temeke alikokuwa amelazwa.

Omar Omar ametamba na muziki wa Mchiriku kwa miaka mingi na wimbo wake wa karibuni zaidi ni "Kupata ni Majaliwa" ambao aliurekodi katika studio ya Dhahabu Records inayomilikiwa na Dully Sykes, ambao aliufanya chini ya prodyuza Pancho.

Mungu ailaze pema peponi roho ya Omar Omar. Amin.

No comments:

Post a Comment