Tuesday, January 8, 2013

MARIA SHARAPOVA SASA "ATOKA" NA "BABY FEDERER"

Boifrendi mpya wa Maria Sharapova, Grigor Dimitrov a.k.a Baby Federer

Maria Sharapova

KAMA hujawahi kumsikia Grigor Dimitrov, utamfahamu hivi punde tu.

Kijana huyo wa Bulgaria mwenye umri wa miaka 21 ni mcheza tenisi anayeinukia.

Akipachikwa jina la utani la "Baby Federer" kutokana na kucheza kwa staili ya kumuiga Roger Federer, Dimitrov tayari yumo ndani ya Top-50 za viwango vya ubora wa tenisi, ambayo bila ya shaka ameingia baada ya kufuzu kucheza fainali za michuano ya Australian Open.

Na kilicho muhimu katika kulitambua jina la Dimitrov (angalau kwa sasa), ni kwamba anatoka na nyota wa mchezo huo Maria Sharapova.

Uvumi ulianza kuzagaa tangu wawili hao walipopigwa picha wakiwa pamoja mjini Milan mwezi uliopita, na wikiendi hii mtangazji wa ESPN, Darren Rovell, alithibitisha kuhusu mahusiano ya wawili hao kwenye Twitter.

Dimitrov amefananishwa na Federer kutokana na upigaji wa mpira wake ukiwamo wa kupiga kwa nyuma. Pia amekuwa akifundishwa na kocha wa zamani wa Federer, Peter Lundgren.

Sharapova (25) alichumbiwa na nyota wa zamani wa NBA, Sasha Vujacic kabla wawili hao kuachana mwaka 2012.


No comments:

Post a Comment