Saturday, January 26, 2013

EL CLASSICO JUMATANO... MOURINHO KUWAKOSA CASILLAS, PEPE, RAMOS, DI MARIA, COENTRAO

Jose Mourinho

WAKATI kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho akijandaa na mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Santiago Bernabéu Jumatano, kocha huyo anakabiliwa ukweli mgumu kuingia kwenye mechi hiyo bila ya nyota wake walio majeruhi Iker Casillas na Pepe, pamoja na waliofungiwa Sergio Ramos, Fabio Coentrao na Angel Di María.

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka la Hispania imewafungia mechi moja Coentrao na Di María, ambao walitolewa kwa kadi nyekundu wakati wa mechi yao ya marudiano ya robo fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Valencia. Wawili hao watakosa mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Barça kwenye Uwanja wa Santiago Bernabéu lakini watakuwa huru kucheza mechi ya marudiano kwenye Uwanja wa Nou Camp..

Casillas – ambaye amefanyiwa upasuaji wa mkono mapema jana baada ya kuumia dhidi ya Valencia - na beki Mreno Pepe – ambaye hivi karibuni alifanyiwa upasuaji wa kutibu majeraha ya enka - hawatacheza mechi zote mbili.

Hata hivyo, Ramos anaruhusiwa kucheza mechi yao ya La Liga wikiendi hii dhidi ya Getafe, lakini bado anatakiwa kutumikia mechi moja zaidi kutokana na adhabu ya kufungiwa mechi tano. Beki huyo mzaliwa wa Sevilla ametumikia adhabu ya kufungiwa mechi nne kutokana na kumbwatukia refa. Mechi moja iliyobaki ambayo inatokana na kutolewa kwa kadi mbili za njano dhidi ya Celta de Vigo ni lazima aitumikie katika michuano husika ya Kombe la Mfalme.

No comments:

Post a Comment