Wednesday, January 9, 2013

MWOSHA-MAGARI ATUMIA TWITTER KUMDAI DEMBA BA MALIPO YAKE
Southampton v Chelsea - FA Cup Third Round
Demba Ba
MUOSHA magari mwenye hasira ametumia ukurasa wake Twitter kumtaka Demba Ba amlipe paundi 40 (Sh. 100,000) baada ya straika huyo "kutoweka" kufuatia kuhamia Chelsea.

Ba, ambaye alikamisha uhamisho wake wa paundi milioni 7 wa kujiunga na Chelsea wiki iliyopita, amewaacha mashabiki wengi wa Newcastle wakiwa wamefadhaika kutokana na kulazimisha uhamisho huo, lakini shabiki mmoja yeye ana sababu tofauti ya kukasirika.

Lee Donnelly – mfanyakazi wa kampuni ya LJD Valet – amedai kwamba aliosha gari ya Ba kabla nyota huyo hajaelekea London kujiunga na Chelsea, na kwamba hakuleta pesa tangu wakati huo.

Donnelly alisema anamdai Ba paundi 40, na akatumia ukurasa wa Twitter wa mchezaji huyo aliouweka kwa ajili ya kuwasiliana na mashabiki wake wa #askba kwa ajili ya kujaribu kuomba malipo yake.
The fan took to Twitter during a #askba chat to request the money (Picture: Twitter)
Meseji iliyoandikwa ya kumdai malipo Demba Ba
‘#askba utanilipa pesa yangu paundi 40 kwa kuosha gari lako?,’ aliandika shabiki huyo.

Kisha akaendelea kumtaka Ba aangalie uhalisia wa mambo, akimkumbusha kwamba paundi 40 si kitu katika paundi 90,000 kwa wiki anazodaiwa kulipwa Stamford Bridge.

‘#AskBa pesa ninayokudai ni asilimia 0.0001% mshahara wako wa siku moja, nilipe Ba"


No comments:

Post a Comment