Wednesday, January 9, 2013

MESSI AWAKERA MASHABIKI WA RONALDO KWA KUTOMTAJA NYOTA WAO WAKATI AKISHUKURU KWA TUZO

Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, Andres Iniesta wa Barcelona na Lionel Messi wa Barcelona wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya wanaowania tuzo za FIFA za Ballon d'Or kwenye ukumbi wa Congress House mjini Zurich, Uswisi Januari 7, 2013.
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, Andres Iniesta wa Barcelona na Lionel Messi wa Barcelona wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya wanaowania tuzo za FIFA za Ballon d'Or kwenye ukumbi wa Congress House mjini Zurich, Uswisi Januari 7, 2013.
Lionel Messi wa Barcelona akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya wanaowania tuzo za FIFA za Ballon d'Or kwenye ukumbi wa Congress House mjini Zurich, Uswisi Januari 7, 2013.

Hili tuzo ntalichukua mimi... Lionel Messi wa Barcelona akiangalia tuzo ya Ballon d'Or wakati akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya wanaowania tuzo za FIFA za Ballon d'Or kwenye ukumbi wa Congress House mjini Zurich, Uswisi Januari 7, 2013.

(Kutoka kushoto kwenda kulia) Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, Andres Iniesta wa Barcelona na Lionel Messi wa Barcelona pamoja na Vicente del Bosque, kocha wa timu ya taifa ya Hispania na Pep Guardiola, kocha wa zamani wa Barcelona wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya wanaowania tuzo za FIFA za Ballon d'Or kwenye ukumbi wa Congress House mjini Zurich, Uswisi Januari 7, 2013.
Radamel Falcao wa Colombia na Lionel Messi wa Argentina wakisalimiana wakati wa kuwasili katika zulia jekundu kabla ya kuanza kwa sherehe za tuzo za FIFA za Ballon d'Or kwenye ukumbi wa Congress House mjini Zurich, Uswisi Januari 7, 2013.

Kumbe alicheka pia... Messi akifurahi wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wa kabla ya sherehe za tuzo

MASHABIKI wa Cristiano Ronaldo waliachwa wakiwa hawajafurahishwa na hotuba ya kushukuru kwa ushindi wa tuzo ya Ballon d'Or iliyotolewa na nyota wa Barcelona, Lionel Messi.

Gazeti la Hispania la Punto Pelota limeripoti kuwa mashabiki hao hawakufurahishwa na kitendo cha Messi kutomtaja hasimu wake wa Real Madrid, Ronaldo katika hotuba yake fupi ya kushukuru kwa tuzo hiyo huku akiwashukuru "wote katika dunia ya soka isipokuwa Mreno".

Wachambuzi wa wamesema mvutano baina ya wawili hao umekuwa mkubwa kuliko ulivyokuwa katika tuzo za mwaka jana, "ungeweza kuona kwa namna walivyokuwa wakipata shida hata kutazamana" wakati wa maandalizi ya pamoja ya yale wanayotakiwa kufanya ukumbini siku ya tukio.

Wanahabari wengi pia hawakufurahishwa na tabia za Messi katika mkutano na wanahabari wa kabla ya sherehe. Ronaldo alikuwa muwazi katika majibu yake, wakati Messi alionekana kutovutiwa kuwapo hapo na alitumia muda wake mwingi akiangalia simu yake ya mkononi.

No comments:

Post a Comment