Tuesday, January 8, 2013

MESSI AMZUNGUKA MARA MBILI RONALDO KWA KURA

Messi akipozi na tuzo yake ya nne ya Ballon d'Or

Messi akishukuru baada ya kupokea tuzo yake ya nne ya Ballon d'Or

Messi (kushoto) akiwa na mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike wa Dunia, Abby Wambach wa Marekani

Messi (kushoto) akipozi na Rais wa FIFA, Sepp Blatter (katikati) na mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike wa Dunia, Abby Wambach wa Marekani

Messi, Iniesta na Ronaldo wakipanda stejini

Messi (kushoto) akimsalimia mshereheshaji wa tuzo hizo

Fabio Cannavaro (wa pili kulia) akimkabidhi Lionel Messi tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia 2012

LIONEL Messi alishinda tuzo ya FIFA Ballon d'Or 2012 kwa mwaka wa nne mfululizo baada ya kupata kura asilimia 41.6, ambazo ni takriban mara mbili ya kura alizopata mpinzani wake wa karibu Cristiano Ronaldo aliyepata 23.6% na Andres Iniesta (10.9%).

Messi alishinda kura za sekta zote tatu zinazopiga kura za kuamua mshindi wa tuzo hiyo ya Mwanasoka Bora wa Dunia. Muargentina huyo aliongoza katika kura zilizopigwa na manahodha wa timu za taifa, zilizopigwa na makocha wa timu za taifa na hata zilizopigwa na wawakilishi wa vyombo vya habari, na katika 'sekta' ya tatu ndipo ambapo Ronaldo alipomkaribia Messi.

Nafasi ya nne ilikwenda kwa nyota wa FC Barcelona, Xavi Hernandez, ambaye alimzidi straika wa Colombia, Radamel Falcao (Atletico de Madrid) na nahodha wa timu ya taifa ya Hispania na Real Madrid, Iker Casillas.

Pirlo, Drogba, Van Persie na Ibrahimovic walikamilisha Top 10 wakati Wahispania wengine Xabi Alonso alishika nafasi ya 11, Sergio Ramos 18, Busquets 20 na Pique 21.

Tuzo ya kocha bora ilienda kwa Vicente Del Bosque aliyempiku kocha Jose Mourinho na Mhispania Pep Guardiola. Kocha wa huyo wa timu ya taifa ya Hispania alipata kura asilimia 34.51 akifuatiwa na Mourinho (20.49%) na kocha wa zamani wa Barcelona, Guardiola (12.91%).

TOP 10 WANASOKA BORA WA MWAKA 2012

1. Lionel Messi (Barcelona, Argentina)

2. Cristiano Ronaldo (Real Madrid, Ureno)

3. Andres Iniesta (Barcelona, Hispania)

4. Xavi Hernandez (Barcelona, Hispania)

5. Radamel Falcao (Atletico Madrid, Colombia)

6. Iker Casillas (Real Madrid, Hispania)

7. Andrea Pirlo (Juventus, Italia)

8. Didier Drogba (Chelsea/Shanghai Shenhua, Ivory Coast)

9. Robin Van Persie (Arsenal/Manchester United, Uholanzi)

10. Zlatan Ibrahimovic (AC Milan/PSG, Sweden)
 


No comments:

Post a Comment