Saturday, January 5, 2013

MARCELO AREJEA UWANJANI MAPEMA KULIKO ILIVYOTARAJIWA

Marcelo (kulia) akiwa na kocha Mourinho katika siku yake ya kwanza mazoezini tangu alipoumia Oktoba 14, 2012

MARCELO amerejea uwanjani kwa mara ya kwanza tangu alipoumia mguu wake wa kulia Oktoba 14 na kufanyiwa upasuaji siku tano baadaye mjini Amsterdam. Marcelo amerejea mapema wiki mbili pungufu ya muda uliotarajiwa, kwani alitarajiwa angerejea katikati ya mwezi huu.

Na amefuzu vyema vipimo vya awali, ingawa kocha Jose Mourinho hatajihatarishia kwa kumchezesha sasa, ila kama ataendelea kupona haraka hivi anaweza kusafiri na timu kwenda kuikabili Pamplona katika Kombe la Mfalme, ingawa anatarajiwa zaidi kurejea dhidi ya Valencia kwenye Uwanja wa Mestalla Januari 20.

Jose Mourinho anafurahia kurejea kwa beki wake chaguo la kwanza upande wa kushoto, hasa hivi sasa kwamba Fabio Coentrao anapitia moja ya vipindi vyake vibaya zaidi tangu alipowasili Real Madrid. Mreno huyo amemchefua kocha Mourinho kwa sababu bado anajifua gym kutokana na maumivu ya misuli aliyoyapata dhidi ya Espanyol, ambayo hayajaisha licha ya mapumziko ya Krismasi. Jambo hilo litamfanya Mourinho ampokee kwa mikono miwili Marcelo.

Licha ya kwamba amerejea mapema kuliko ilivyotarajiwa, lengo la Mourinho ni kwamba Marcelo awe fiti kwa ajili ya mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Manchester United.

No comments:

Post a Comment