Saturday, January 5, 2013

CHAMAKH ATIMKA ARSENAL... ATUA WEST HAM KWA MKOPO

Marouane Chamakh
Straika wa Arsenal, Marouane Chamakh amejiunga na West Ham kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.

Straika huyo wa kimataifa kutoka Morocco, 28, amekuwa akihaha kupata namba katika kikosi cha Arsenal tangu atue kwa uhamisho huru kutoka Bordeaux mwaka 2010.

Hata hivyo, West Ham wamempa Chamakh nafasi ya kuokoa kipaji chake

Kusajiliwa kwa Chamakh kumekuja baada ya ujio wa Joe Cole, al;iyekamilisha uhamisho wake kwenda West Ham akitokea Liverpool kwa mkopo wa miezi 18 mapema jana.

Chamakh alikuwa tishio Ufaransa, akifunga magoli 79 katika mechi 293 alizoichezea Bordeaux, lakini ameifungia Arsenal goli nane tu katika Ligi Kuu ya England tangu ajiunge na klabu hiyo - na bado hajacheza katika mechi yoyote ya ligi kuu msimu huu.

Mechi tatu kati ya nne alizocheza msimu huu ni za Kombe la Capital One, na alifunga magoli mawili wakati Arsenal ikiisambaratisha Reading kwa kuifunga mabao 7-5 mwezi Oktoba.

No comments:

Post a Comment