Tuesday, January 15, 2013

LIVERPOOL WAMTAKA VALDES AMBADILI REINA

Victor Valdes

KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers yuko tayari kumsajili kipa wa Barcelona, Victor Valdes.

Gazeti la People la Uingereza limesema Valdes atakuwa amebakisha miezi 12 katika mkataba wake mwisho wa msimu huu na mazungumzo ya mkataba mpya yamekwama.

Suala lake limewavutia watu wa Anfield, ambako Pepe Reina – ambaye yuko ya Valdes katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania – kwa mara nyingine amejadiliwa huku pia Arsenal wakisemekana kuvutiwa naye.

Manchester City pia wanamuangalia Valdes, ingawa si jambo rahisi kwa kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 kuchukua namba kwa Kipa Na.1 wa Etihad, Joe Hart.

No comments:

Post a Comment