Tuesday, January 15, 2013

DIAME SI MCHEZAJI WA AINA YA ARSENAL, ASEMA KOCHA WA WEST HAM

Mohamed Diame wa West Ham United akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Chelsea wakati wa mechi yao ya Ligi kuu ya England kwenye Uwanja wa Boleyn Ground mjini London, England Desemba 1, 2012.

KOCHA wa West Ham United, Sam Allardyce amedhamiria kumbakisha kiungo wa ulinzi Momo Diame.

Kiungo huyo wa Senegal, anatakiwa na Arsenal.

Lakini Allardyce amesema: "Daima unapata hofu ya kuwapoteza wachezaji wako lakini hatujaletewa ofa yoyote kutoka Arsenal kwa ajili ya Mo Diame. Sioni mahala gani atafiti kwenye kikosi chao."

Ripoti za uvumi zimedai kwamba Arsenal wameandaa ofa ya paundi milioni 3.5 kwa ajili ya kumnasa kiungo huyo.

No comments:

Post a Comment