Wednesday, January 16, 2013

CARRICK HAPIGI "TACKLE", ASEMA KOCHA WA WEST HAM

Michael Carrick

KOCHA wa West Ham United, Sam Allardyce amesema ni mara chache sana unaweza kumuona kiungo wa Manchester United, Michael Carrick "aki-tackle" kuchukua mpira kutoka kwa mpinzani.

Allardyce amesema nyota huyo wa Man United anafahamika zaidi kwa uwezo wake mkubwa wa kuusoma mchezo na kuiba pasi kuliko kucheza "tackle" tofauti na ilivyokuwa enzi zao (Allardyce) wakati akipiga soka.

Allardyce alisema: "Ukiangalia na kuuliza wako wapi viungo maarufu kwa '­tackling' kama Roy Keane, Nicky Butt na Bryan Robson utaona ni wachcahe sana.

"Leo mambo ni kuusoma mchezo, kuingia katikati ya pasi za wapinzani na kuiba mpira.

"Je, Michael Carrick ni mfano mzuri wa hilo? Nadhani ndiyo.

"Mambo ya 'tackling' ni kama yameshakufa kabisa. Sisi makocha hatufundishi tena kupiga 'tackle', ni kusoma mchezo, vizia, iba mpira.

"Je, FIFA na UEFA wanataka kupiga marufuku tackling? Inaonekana jibu ni ndiyo, lakini soka ni mchezo wa mgongano."

No comments:

Post a Comment