Tuesday, January 15, 2013

KOMPANY AFUTIWA KADI NYEKUNDU

Vincent Kompany wa Manchester City (kushoto) akitoka uwanjani baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu na refa Mike Dean (kulia) wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England Januari 13, 2013. Man City walipiga 'mtu' 2-0.

MANCHESTER City wameshinda rufaa yao dhidi ya kadi nyekundu aliyopewa nahodha Vincent Kompany katika kipindi cha pili cha mechi yao waliyoshinda 2-0 dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates.

Beki huyo wa kati alitolewa na refa Mike Dean kwa 'tackle' aliyocheza dhidi ya Jack Wilshere lakini Chama cha Soka cha England (FA) kimetengua maamuzi hayo.

Kompany angefungiwa kucheza mechi tatu dhidi ya Fulham na QPR katika Ligi Kuu ya England, na moja ya raundi ya nne ya Kombe la FA dhidi ya Crystal Palace au Stoke.

No comments:

Post a Comment