Tuesday, January 15, 2013

EMMANUEL OKWI ATIMKA RASMI SIMBA... ADAIWA KUTUA ETOILE DU SAHEL YA TUNISIA KWA DAU KUFURU BONGO LA SH. MILIONI 472


Chezea Okwi weye...! Straika Okwi wa Simba (kulia) akiwafungisha tela mabeki wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam..
Na Mahmoud Zubeiry
Straika wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi wa Simba ameuzwa kwa klabu ya Etoile du Sahel ya Ligi Kuu ya Tunisia kwa dola za Kimarekani 300,000 (Sh. milioni 472)

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe, ameiambia bongostaz.blogspot.com kuwa, Okwi amekamilisha vipimo na kila kitu na tayari amesaini mkataba.

“Tunasubiri kulipwa fedha zetu tu, viongozi watakwenda Tunisia kuchukua fedha za mauzo ya mchezaji huyo,”alisema Poppe.

Okwi amekuwa akipiga chenga kuripoti kambini Simba SC na alikuwa hata hapokei simu za viongozi wa klabu hiyo kila alipopigiwa.

Kufuatia hatua hiyo, uongozi ulimuengua kwenye programu ya safari ya Oman na sasa inabainika ametua Sahel.

Okwi, aliyezaliwa Desemba 25, mwaka 1992 aliisajiliwa Simba akitoea SC Villa ya Uganda mwaka 2010 akiwa yosso wa miaka 17, akisajiliwa kwa dau la dola za Kimarekani 40,000 (Sh. milioni 63).

Baada ya kumaliza mkataba wake wa awali, Desemba mwaka jana aliongeza mkataba wa miaka miwili na Simba ambao kabla hajaanza kuutumikia, ameamua kuhamia Sahel.


(Bongostaz.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment