Thursday, January 3, 2013

STURRIDGE AKAMILISHA UHAMISHO LIVERPOOL NA KUPEWA JEZI NA. 15

Sasa mtanikoma Chelsea...! Straika Daniel Sturridge akionesha 'uzi' atakaokuwa akivaa baada ya kusaini mkataba mrefu wa kuichezea Liverpool jana Janauri 2, 2013..

Hapa sasa kila kitu shwari. Kazi kwako kijana...! Afisa wa Liverpool akipeana mkono na Sturridge (kulia) baada ya straika huyo kusaini mkataba mrefu wa kuichezea Chelsea jana Januari 2, 2012. 
Liverpool wamekamilisha usajili wa straika wa kimataifa wa England, Daniel Sturridge waliyemnasa kutoka Chelsea.

Straika huyo mwenye miaka 23 alifanyiwa vipimo vya afya na kufuzu wiki iliyopita kwenye kituo cha Melwood na jana akakamilisha masuala binafsi ya mkataba wake wa muda mrefu.

Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers alimchukulia Sturridge kuwa chaguo lake la kwanza wakati wa kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo la Januari, na amefurahi kuona kuwa ndoto zake zimetimia haraka.

"Nimefurahi kuwa hapa," amesema Sturridge, ambaye klabu yake mpya imethibitisha kuwa atavaa jezi namba 15.

Taarifa zimedai kuw Liverpool ililazimika kuilipa Chelsea ada ya uhamisho ya paundi za England milioni 12 ili kumnasa straika huyo.

No comments:

Post a Comment