Saturday, January 26, 2013

KAKA AENDE MILAN, ASEMA MOURINHO

Kaka

KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho amesema Kaka anapaswa kurejea katika klabu yake ya zamani ya AC Milan.

Mourinho anaamini kwamba kiungo huyo Mbrazil mwenye umri wa miaka 30 atakuwa na furaha zaidi akirejea San Siro.

“Awali ya yote nataka Kaka awe na furaha,” Mourinho aliuambia mkutano na waandishi wa habari. "Nadhani Milan patakuwa suluhisho sahihi kwake.

"Kwa sasa hatahivyo, ataendelea kuwa mchezaji wa Madrid."

No comments:

Post a Comment