Saturday, January 26, 2013

IKER CASILLAS AFANYIWA UPASUAJI WA MKONO... DOKTA ASEMA ATALAZIMIKA KUKAA NJE YA UWANJA KWA MIEZI KATI YA MIWILI NA MITATU... SASA KUZIKOSA MECHI ZOTE ZA REAL MADRID DHIDI YA BARCELONA KATIKA EL CLASICO YA KOMBE LA MFALME NA PIA DHIDI YA MANCHESTER UNITED KATIKA LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA... REAL WAMSAJILI KIPA DIEGO LOPEZ WA SEVILLA KUZIBA NAFASI YAKE...!

Mambo dole tupu ... naendelea vizuri washkaji. Ila naomba dua zenu nipone haraka! Casillas anavyoonekana akiwa hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji jana Ijumaa Januari 25, 2013.
Msihofu... nakwamba mtamsahau huyo Casillas wenu! Kipa Diego López anatua Real Madrid akitokea Sevilla kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Casillas. 
MADRID, Hispania
Daktari aliyemfanyia upasuaji kipa Iker Casillas wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, amesema kuwa nahodha huyo wa timu hizo mbili anaweza kuwa nje ya uwanja kwa kati ya miezi miwili hadi mitatu, kipindi ambacho ni kirefu zaidi ya vile ilivyotarajiwa.

"Upasuaji umeenda vizuri sana", Dokta Del Cerro aliviambia vyombo vya habari baada ya kufanikiwa kumfanyia upasuaji Iker Casillas, ambaye alivunjika kifupa cgha mkono katikati ya wiki wakati wa mechi yao ya marudiano ya Kombe la Mfalme dhidi ya Valencia Jumatano.

"Mfupa uliovunjika umerekebishwa na vyuma viwili vimewekwa ili kuhakikisha kwamba mkono unarudia katika hali yake ya kawaida. Upasuaji ulikwenda vizuri sana. Atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha kati ya wiki nane hadi kumi na mbili, ingawa ni vizuri kusubiri na kuona anavyoendelea kabla ya kukadiria," aliongeza daktari huyo wa hospitali iliyopo   Madrid ya Beata María Ana.

De Cerro alithibitisha vilevile kuwa Casillas atalazimika kuvaa 'hogo' kwa wiki tatu, na leo (Jumamosi Januari 26) atarudi tena hospitali kuangaliwa maendeleo ya jeraha lake.
"...misumari itaachwa kwenye mkono wake. Ina urefu wa milimita 17 na upana wa milimita mbili", alisema Dokta Del Cerro.

Taarifa hizo kuhusiana na upasuaji wa mkono wa Casillas zinamaanisha kuwa nahodha huyo wa Real atazikosa mechi kadhaa muhimu za klabu yake, zikiwambo mbili zitakazoanza Jumatano ijayo za nusu fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Barcelona na pia, nyingine mbili za Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Manchester United zitakazochezwa mwezi ujao.  

Kipa Diego López wa klabu ya Sevilla ambaye alianzia soka lake akiwa na Real amesajiliwa kuziba nafasi ya majeruhi Casillas.

Kipa Lopez aliwahi pia kudakika Villareal.

No comments:

Post a Comment